BARCELONA WAJIPA MATUMAINI YA MESSI KUENDELEA KUBAKI KIKOSINI HADI ZAIDI YA 2018



BARCELONA WAJIPA MATUMAINI YA MESSI KUENDELEA KUBAKI KIKOSINI HADI ZAIDI YA 2018
RAIS wa Barcelona, Josep Maria Bartomeu amesema kwamba ana uhakika staa wao, Lionel Messi ataongeza mkataba hadi zaidi ya mwaka 2018, lakini akasema kuwa hakuna mazungumzo kuhusu hatma ya kocha wao, Luis Enrique.

Hadi sasa mshindi huyo wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia, Ballon d'Or ameshatwaa mataji 28 akiwa na Barca, lakini amebakiza miaka miwili kwenye mkataba wake na klabu hiyo ya Camp Nou.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 29, hivi karibuni alikosa kuonja ladha ubingwa akiwa na timu ya taifa baada ya Argentina kufungwa mikwaju ya penati na Chile katika mechi ya fainali ya michuano ya Kombe la Copa America Centanario.

Baada ya kukosa taji hilo, Messi aliamua kustaafu kuichezea timu hiyo nah ii ilikuwa ni mara ya nne kwa staa huyo kukosa ubingwa katika mechi ya fainali akiwa na Argentina.

Hata hivyo akizungumza juzi, Bartomeu alisema kuwa ana uhakika nyota huyo ataendelea kukaa kwa muda mrefu Barca.

"Sote tunamfahamu Leo Messi. Mara zote huwa anapenda kushinda na ndio maana akaamua kustaafu kuichezea timu ya taifa. Huo ni mjadala binafsi," alisema rais huyo.
Messi ni mali ya Barca na tumeshamwambia kubaki kwa muda mrefu na vilevile ni balozi wa soka duniani," aliongeza rais huyo.


Alisema kwamba kwa sasa Messi amebakiza muda wa miaka miwili kwenye mkataba wake na hivyo ana uhakika ataweza kuongeza muda.


Comments