BAADA YA MICHUANO YA EURO KUMALIZIKA, HII NDIO TOP 10 YA WACHEZAJI WALIONG’ARA





BAADA YA MICHUANO YA EURO KUMALIZIKA, HII NDIO TOP 10 YA WACHEZAJI WALIONG'ARA
Ronaldo vs Hungary

Kufuatia ushindi wa Ureno wa bao 1-0 dhidi ya Ufaransa na kutwaa kombe la Euro 2016, UEFA walitoa kikosi rasmi bora cha mashindano.

Kama ilivyoada si kila mtu alifurahishwa na kikosi hicho kilichochaguliwa na jopo la watu 13 wakiwemo Sir Alex Ferguson, Gareth Southgate na David Moyes.

Kwa kuona hilo, mtandao wa 101greatgoals.com umetoa kikosi chao bora cha michuano hiyo kinachoundwa na wachezaji 10.

Lakini Orodha hii inawapendelea zaidi wachezaji wanacheza kuanzia nafasi za kiungo na ushambuliaji. Hivyo basi wachezaji kama Bacary Sagna (Ufaransa), Giorgio Chiellini (Italy) na Raphael Guerreiro (Ureno) wameachwa.

  1. Kevin De Bruyne (Ubelgiji)

De Bruyne aliondoka na kiwango chake bora kutoka Ligi ya England na kukihamishia kwenye Michuano ya Euro. Licha ya kwamba timu yake ilitolewa hatua ya nusu fainali na Wales, De Bruyne alitoa pasi tatu za magoli. Staa huyo wa Manchester City alitengeneza nafasi 23 kwa timu yake, nyingi zaidi ya mchezaji yeyote kwenye michuano.

  1. Aaron Ramsey (Wales)

Baada ya kutokuwa na msimu mzuri kwenye ligi ya EPL na klabu yake ya Arsenal, Aaron Ramsey alikuja kivingine kwenye Michuano ya Euro. Ndiye mchezaji aliyeongoza kwa kutoa pasi nyingi za magoli. Alifunga goli la kwanza kwa Wales katika mchezo dhidi ya Russia kweye hatua ya makundi. Aliukosa mchezo muhimu wa nusu fainali dhidi ya Ureno na ama hakika pengo lake lilionekana.

  1. Hugo Lloris (Ufaransa)

Mpaka hatua ya robo fainali, Lloris alikuwa hajaruhusu goli lolote kwa njia ya kawaida. Mlinda lango huyo wa Spurs alifanya kazi kubwa ikiwa ni pamoja na kuokoa michoamo ya maana katika michezo mbalimbali katika michuano hiyo. Ndiye aliyekuwa nahodha wa Ufaransa kwenye michuano.

  1. Toni Kroos (Ujerumani)

Pengine watu wengine hawawezi kuona mchango wake kwenye michuano hii, lakini Toni Kroos alhusika katika pasi nyingi maridadi bila ya kusahau ndiye alikuwa mpigaji wa mipira yote ya adhabu ndogo na kona (set-pieces). Kroos alipiga pasi 642 kwenye michuano na kupata na asilimia 92% katika ubora wa pasi.

  1. Pepe (Ureno)
  1. Pepe (Ureno)

Bila shaka yoyote huyu ni moja wa mabeki bora kwenye michuano ya Euro mwaka huu. Pepe aliiongoza kwa umahiri mkubwa safu ya ulinzo ya Ureno na kuruhusu bao moja tu kwenye michezo ya hatua ya mtoano. Alikuwa yuko radhi kuweka mwili wake kuzuia mpira kufika langoni kwake au kupiga 'tackle',. Ndiye beki aliyefanya 'interceptions' nyingi kwenye michuano hii (16).

  1. Eden Hazard (Ubelgiji)

Alikuwa kwenye kiwango bora sana katika michuano hii. Watu wengi walianza kumbeza kwamba kiwango chake kimeshuka kutokana na kutokuwa na msimu mzuri wa ligi mwaka 2015/16. Kwenye mchezo wa  16 bora dhidi ya Hungary ambapo Ubelgiji walishinda mabao 4-0, Hazard alionesha uwezo mkubwa sana. Ametia amefunga goli moja na kutoa assist 1 kwenye magoli 9 ya Ubelgiji kwenye Michuano ya Euro.

  1. Dimitri Payet (Ufaransa)

Ndiye mfungaji wa goli la ushindi katika mchezo wa ufunguzi wa kati ya Ufaransa na Romania, goli ambalo lilikuwa ni hatari sana. Akicheza kutokea upande wa kushoto, Payet alitengeneza nafasi 21 kwa wachezaji wenzake, akizidiwa mbili na De Bruyne. Kwa ujumla katika michezo yote, Payet alionesha kiwango cha hali ya juu licha ya kufanyiwa sub katika mchezo wa fainali dhidi ya Ureno.

  1. Gareth Bale (Wales)

Bale alifunga kwenye michezo yote ya hatua ya makundi, yakiwemo yake ya mipira ya adhabu ndogo 'free-kicks' dhidi ya Slovakia na England. Alionesha kiwango cha hali ya juu katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Ureno licha ya timu yake kufungwa magoli 2-0. Alikuwa moja ya wachezaji muhimu sana kwenye kikosi cha Wales.

  1. Cristiano Ronaldo (Ureno)

Hakuna mchezaji alyepiga mashuti mengi zaidi langoni mwa timu pinzani kama Cristiano Ronaldo ambaye alipiga mashuti 46. Licha ya kutokuwa na kiwango bora katika michezo miwili ya awali katika hatua ya makundi ikiwemo kukosa penati katika mchezo dhidi ya Austria.  Lakini baadaye ali-recover na kuonyesha kile alichozoea kufanya. Alifunga magoli 3 na kutoa pasi tatu za magoli. Aliumia kwenye mchezo wa fainali lakini mchango wake wakati akiwa kwenye benchi ilikuwa ishara kubwa ya mafanikio ya Ureno katika mchezo huo ambapo waliweza kushinda kwa bao 1-0 dhidi ya wenyeji Ufaransa.

  1. Antoine Griezmann (Ufaransa)

Griezmann-FranceAmefunga magoli 6 na kuwa mfungaji bora wa michuano. Mchezo ambao ulikuwa bora sana kwake ni ule dhidi ya Iceland, ambapo alifunga goli moja na kutoa assists mbili.



Comments