MIAMBA wa soka Hispania, klabu ya Atletico Madrid imedhamiria kuimarisha safu yao ya ushambuliaji kuelekea msimu mpya na tayari imeandaa ofa kwa mastraika watatu ambao wamehusishwa kutimka kwenye klabu zao hivi karibuni.
Atletico inaangalia uwezekano wa kunasa saini ya mmoja kati ya Pierre Emerick Aubameyang, Gonzalo Higuain au Diego Costa ambao wana thamani kati ya euro mil 50 hadi 60.
Klabu hiyo itakutana na wakati mgumu kwani miamba mingine nayo inawatolea macho washambuliaji hao ikiwemo Real Madrid, Manchester United, Manchester City na Chelsea.
Comments
Post a Comment