KLABU ya Arsenal imekamilisha nipango ya kumsajili mlinzi kinda wa Bolton Wanderers, Rob Holding ambaye ameonyesha ukomavu mkubwa dimbani.
Mchezaji huyo mwenye miaka 20 alikuwa mhimili wa Bolton msimu uliopita akicheza mechi 30 na kufunga bao moja.
Habari za uhakika zinasema kuwa Arsenal wamemtengea kiasi cha pauni mil 2 ambazo zilikuwa zikihitajiwa na Bolton Wanderers.
Mchezaji huyo licha ya kutokuwa na uzoefu, amekuwa akijituma na alianza kuonyesha ukomavu katika kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 21 ya England.
Comments
Post a Comment