KIWANGO cha kinda Ousmane Dembele wa timu ya Lennes ya Ufaransa kinawaingiza vitani vigogo wa soka barani Ulaya, Arsenal na Barcelona ambao wote wanasaka saini yake.
Vita ya timu hizo inatokana na kila mmoja kutangaza dau nono kwa kinda huyo mwenye umri wa miaka 18 ambapo Barca wameweka mezani dau la pauni mil 24, wakati Arsenal wametangaza ofa ya pauni mil 25.
Dembele ambaye ni kijana mwenye kipaji cha kucheza kama straika namba 10, alianza kung'ara katika soka la kulipwa mwezi Novemba mwaka jana na kufunga mabao 17 katika michuano ya Ligue 1.
Katika hali ya kuamini ni mchezaji wa kiwango, klabu yake ya Lennes ilimpa mkataba wa miaka mitatu mnao mwezi Oktoba mwaka jana akishawishiwa na mchezaji wa zamani wa Arsenal, Mikael Silvestre.
Arsenal waliingia katika mbio za kumwania straika huyo baada ya kocha Arsenae Wenger kuamua kumfuatilia kwa kipindi kirefu kwa kumtumia mkuu wa kitengo cha kufuatilia wachezaji cha Emirates, Steve Rowley.
Steve Rowley ameripotiwa kufanya safari za mara kwa mara katika kila mechi ambayo Dembele anacheza na kuridhishwa na kiwango chake na taarifa kumfikia Arsene Wenger.
Kwa upande wa Barcelona, wamekuwa wakimtumia mkurugenzi wa michezo, Robert Fernandez ambaye amesafiri mara kadhaa kwa ajili ya kufuatilia kiwango cha straika huyo kinda.

Comments
Post a Comment