ANTONIO CONTE AWASHANGAA WANAODHANI DIEGO COSTA ATAONDOKA CHELSEA




ANTONIO CONTE AWASHANGAA WANAODHANI DIEGO COSTA ATAONDOKA CHELSEA
KOCHA mpya wa Chelsea, Antonio Conte amefunguka na kusema anawashangaa wanaodhani mshambuliaji mahiri Diego Costa ataondoka.

Conte alisema Diego Costa yupo katika mipango yake na anatarajia ndiye atakayeongoza mashambulizi ya matajiri hao msimu ujao.

"Ni kichekesho kusema Costa ataondoka Chelsea kurudi Atletico Madrid, sidhani kama tunaweza kumuacha mchezaji mahiri kama yeye bila sababu za msingi kwa wakati huu," alisema.

Hofu ya mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Hispania mwenye asili ya Kibrazil kurejea atletico ilikolezwa na klabu hiyo kwamba wanamkaribisha kwa mikono miwili iwapo atataka kurejea.

Conte amekata mzizi wa fitina siku chache kabla ya kuanza Ligi Kuu England ambapo amesema Costa ameshajiunga na wenzake kuanza maandalizi ya msimu mpya na ana furaha.

Alisema, anaamini wachezaji wote wa Chelsea walicheza chini ya kiwango msimu uliopita na hiyo ilitokana na uchovu.

"Kama utakumbuka wachezaji wa Chelea walicheza mechi zote za Ligi ya Mabingwa Ulaya walikofikia nusu fainali, walitwaa ubingwa wa Ligi Kuu na Kombe la FA, pia walifika fainali Kombe la Ligi, hivyo walichoka sana," alisema Conte.

Aliwasihi mashabiki kuwaunga mkono wachezaji wao akiapa kulirejesha taji la Ligi Stanford Bridge.


Pia amethibitisha Chelsea itashiriki mechi maalum za maandalizi ya msimu mpya ambapo watacheza na Liverpool, Real Madrid na AC Milan mjini Pasadena California; Ann Arbor, Michigan na Minneapolis, Marekani.


Comments