ANTONIO CONTE ASEMA HAONI AIBU KUFUNGWA KWA PENATI


ANTONIO CONTE ASEMA HAONI AIBU KUFUNGWA KWA PENATI
KWA kile ambacho unaweza kusema ni kama karidhika, kocha wa Italia, Antonio Conte amesema kwamba haoni aibu kwa timu yake kufungwa kwa mikwaju ya penati, baada ya kutolewa nje ya michuano ya fainali za mataifa ya Ulaya "Euro 2016" katika hatua ya robo fainali iliyopigwa usiku wa kuamkia jana mjini Boudreaux.

Katika mchezo huo, beki Leonardo Bonucci ndie aliyesawazisha bao la kuongoza lililofungwa na Mesult Ozil ikiwa ni baada ya miamba hao wawili kwenda sare ya bao 1-1 katika muda wa dakika 120.

Wakati Ujerumani, Italia hazijawahi kupigiana penati katika mashindano makubwa, lakini mabingwa wa dunia, Ujerumani wameweka rekodi nzuri ya kutofungwa kwa njia hiyo tangu mwaka 1976.

Hii ni kutokana na kwamba rekodi haikubadilika hadi mwisho wa mtanange huo ambapo ilishuhudiwa wachezaji saba wakishindwa kuziona nyavu.

Alikuwa na Matteo Darmian ambaye aliigharimu timu yake na kumfanya staa mwenye umri wa miaka 26, Jonas Hector akapachika bao la ushindi lililoipeleka Ujerumani katika hatua ya nusu fainali.

"Vijana wamefanya kila kitu dhidi ya kikosi imara," Conte ambaye anaachia nafasi yake kwenda kujiunga na Chelsea kwenye michuano ya Ligi Kuu England, aliuambia mtandao wa Rai Sports.


"Kwa kufungwa kwa njia ya penati na Ujerumani sioni aibu kutokana na kwamba tulipambana na ninajivunia kwa hiki ambacho vijana wamekifanya," aliongeza kocha huyo.


Comments