ANTHONY AINUNIA MANCHESTER UNITED KUMPA ZLATAN IBRAHIMOVIC JEZI YAKE



ANTHONY AINUNIA MANCHESTER UNITED KUMPA ZLATAN IBRAHIMOVIC JEZI YAKE
BAADA ya klabu ya Manchester United kutangaza namba mpya za jezi za wachezaji wao kwa ajili ya msimu wa 2016/17, sasa mtafaruku mkubwa umezuka baada ya Zlatan Ibrahimovic kupewa jezi namba tisa iliyokuwa ikitumiwa na kinda Anthony Martial.

Tayari ilishajulikana wazi kuwa Ibrahimovic angevaa jezi hilo, lakini tangazo la kubadilishwa kwa namba lilitolewa wakati Martial akiwa bado kwenye mapumziko yake, jambo lililoonekana kutomridhisha Mfaransa huyo aliyeamua kuonyesha hasira zake kwenye mtandao wa kijamii.

Matrtial aliamua kufuta urafiki na akaunti rasmi ya Manchester United katika mtandao wa Twitter kutoka ile iliyokuwa ikimuonyesha akishangilia bao na kuweka picha aliyopiga ikiwa na jina lake sambamba na namba tisa.


United ilimsajili mshambuliaji huyo mwaka jana kwa dau linalotabiriwa kupanda hadi euro mil 80 na sasa imemkera kwa kumbadilisha namba na kumpa jezi namba 11 bila ridhaa yake, huku ikidaiwa kuwa huenda hiyo ikawa changamoto ya kwanza atakayokutana nayo Jose vyumba vya kubadilisha nguo.


Comments