ANDRE GOMES AGOMBEWA NA TIMU KUBWA NNE BARANI ULAYA



ANDRE GOMES AGOMBEWA NA TIMU KUBWA NNE BARANI ULAYA
KIUNGO chipukizi wa Valencia, Andre Gomes anagombewa na miamba wa soka barani Ulaya.

Timu nne kubwa barani Ulaya zimewasilisha ofa zikimtaka Gomes ambapo FC Barcelona, Real Madrid, Manchester United na Chelea zote zimeridhia dau la pauni mil 54.


Kiungo huyo mwenye miaka 22 alikuwa kwenye kiwango kizuri msimu uliopita, jambo lililozivutia timu nyingi kumhitaji.


Comments