ANCELOTTI AGOMA KUMUUZA ROBERT LEWANDOWSKI KWA REAL MADRID



ANCELOTTI AGOMA KUMUUZA ROBERT LEWANDOWSKI KWA REAL MADRID
KOCHA wa Bayern Munich, Carlo Ancelotti amesema kuwa hana mpango wa kumuuza staa wake, Robert Lewandowski katika timu ya Real Madrid na amesema kuwa vinara hao wa Ligi ya La Liga hawamtaki straika huyo raia wa Poland.

Kauli ya kocha huyo imekuja baada ya taarifa za hivi karibunikudai kuwa Lewandowski ambaye ameshafunga mabao 47 katika kipindi alichocheza Ligi ya Bundesliga akiwa na Bayern, ana mpango wa kwenda kujiunga na klabu hiyo ya Santiago Bernabeu.

Taarifa hizo zinadai kuwa Real Madrid inapima upepo jinsi ya kukamilisha mkataba wa kumchukua straika huyo wa zamani wa Borussia Dortmund akakipige kwenye michuano hiyo ya La Liga ili kukamilisha safu yake ya ushambuliaji ambayo tayari ina nyota Cristiano Ronaldo, Gareth Bale na Karim Benzema.

Hata hivyo, kocha huyo wa zamani wa Real Madrid, Ancelotti alifunguka juzi akisema kwamba mabingwa hao wa Ligi ya Bundesliga hawatamruhusu mmoja wa hadhina zake kuondoka kwenye klabu hiyo ya Allianz Arena.

"Real Madrid ina wachezaji wengi wazuri kama Benzema, Bale na Ronald. Hata hivyo hawamtaki Lewandowski," Ancelotti aliliambia jarida la Sport Bild.


"Na hata kama wanajisikia kuwa na haja ya kumwitaji Lewandowski, Bayern haiwezi ikamuuza," aliongeza.


Comments