Gazeti la Marca la Hispania limedai kuwa kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane ameiagiza klabu yake kufanya kila wawezalo ili kumsajili kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa.
Zidane anataka kuboresha safu yake ya kiungo cha ukabaji katika kipindi hiki ambacho Casemiro yuko peke yake kwenye eneo hilo.
Kante alijiunga na Leicester kwa pauni milioni 5.6 kiangazi kilichopita akitokea Caen ya Ufaransa.
Comments
Post a Comment