NAHODHA wa timu ya taifa ya England, Wayne Rooney amesema kwamba hana mpango wa kustaafu kuichezea timu hiyo, licha ya kutupwa nje ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Ulaya "Euro 2016".
Straika huyo wa timu ya Manchester United ndie aliyewafanya vijana wa kocha Roy Rodgson kuwa mbele kwa bao moja katika mchezo huo uliopigwa usiku wa kuamkia jana mjini Nice, lakini mabao kutoka kwa nyota Ragnar Sigurdsson na Kolbeinn Sigthorsson wakaipa Iceland ushindi wa mabao 2-1.
Baada ya mchezo huo, kocha Rodgson alitangaza kwa haraka kustaafu, lakini straika huyo, Rooney akasema kuwa hana mpango wa kufuata nyayo za kocha wake.
Kucheza katika mchezo huo dhidi ya Iceland inakuwa ni mechi yake ya 115 sawa na David Beckham, ambao wanashikiria rekodi ya kucheza mechi nyingi katika kikosi hicho cha England.
"Nimewahi kusema kabla ya mashindano haya wakati nilipoulizwa mara nyingi, lakini nasema najivunia kuchezea England na nina hamu na mpango wa kuona nani atakuwa kocha mwingine wa timu hii," alisema Rooney.
"Na kama nitachaguliwa nipo tayari kucheza," aliongeza staa huyo.
Comments
Post a Comment