UNAWEZA kusema ni kama kapagawishwa, straika Wayne Rooney amekiangalia kikosi cha timu ya taifa ya England kitakachokwenda kucheza kwenye michuano ya fainali za Mataifa ya Ulaya "Euro 2016" na kisha akasema kuwa anavyoona ndicho bora tangu aanze kuitumikia timu hiyo.
Nahodha huyo na mfungaji bora, alianza kuichezea timu hiyo Februari, 2003 na tayari ameshaichezea katika mashindano makubwa matano na huku ya sita yakiwa njiani.
Hata hivyo Rooney mwenye umri wa miaka 30 anasema kuwa, anavyoamini kikosi cha sasa atakachosafiri nacho kwenda Ufaransa kinavipiku vyote vilivyopita lakini akasema kuwa wanatakiwa kujifunza kutoka kwa wapinzani.
"Kikosi hiki kina kila kitu cha kuwa bora tofauti na vingine nilivyowahi kuvichezea," staa huyo aliwaambia waandishi wa habari.
"Nadhani hatma ya kikosi cha England sasa ipo wazi. Unaweza kufanya vizuri majira haya ya joto," aliongeza nyota huyo.
Alisema kwamba anavyofahamu wana kikosi kizuri lakini wanachotakiwa kufanya ni kujituma.
Comments
Post a Comment