WAYNE ROONEY ASEMA YEYE NI BORA ZAIDI KWA SASA KULIKO KIPINDI KINGINE CHOCHOTE KILE



WAYNE ROONEY ASEMA YEYE NI BORA ZAIDI KWA SASA KULIKO KIPINDI KINGINE CHOCHOTE KILE
GETTY

WAYNE ROONEY inaingia Euro 2016 Jumamosi usiku huku akisisitiza kuwa yuko katika kiwango kizuri kuliko kipindi kingine chochote kile.

Alhamisi usiku mwandishi mmoja wa Urusi alimnanga nahodha huyo wa England kwa kusema hisia zilizopo kwa mashabiki wa nchi yake ni kwamba  Rooney si yule waliyemzoea.
"Ninajua mchezo wangu umebadilika - lakini kwa maoni yangu, mabadiliko hayo ni kuimarika zaidi kwa soka langu"
Wayne Rooney
Lakini kuelekea mchezo wa kwanza baina ya nchini hizo mbili, Rooney amesisitiza: "Ninajua mchezo wangu umebadilika - lakini kwa maoni yangu, mabadiliko hayo ni kuimarika zaidi kwa soka langu.
"Kila mmoja ana maoni yake, lakini najua ubora wangu. Sijaja hapa kujitetea.
"Maoni ya kuzingatia ni yale yatakayotoka kwa kocha wangu na kwa wachezaji wenzangu. 
"Miezi michache iliyopita nilicheza kama kiungo Manchester United na nadhani naweza kuendelea na soka langu kwenye nafasi hiyo."


Comments