WALES YAPIGIWA CHAPUO UBINGWA WA EURO 2016



WALES YAPIGIWA CHAPUO UBINGWA WA EURO 2016
KIWANGO bora kilichoonyeshwa na timu ya taifa ya Wales, kimefanya wachambuzi wengi wa soka kubadili mitazamo yao na sasa wanaipa nchi hiyo nafasi ya kutinga fainali.

Wales ambayo haikuwa ikipewa nafasi na wengi, imeonyesha soka la hali ya juu ambapo imepoteza mchezo mmoja na kushinda miwili katika hatua ya makundi na hivyo kuwa kinara wa Kundi B.

Hata hivyo mashindano ya mwaka huu yameelezwa kukosa msisimko kutokana na hofu ya mashambulizi ya kigaidi pamoja na mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.


Ufaransa ni moja ya ncchi za Ulaya zenye waislamu wengi, hivyo inaaminika kuwa mashabiki wengi waislamu wa ndani na nje ya Ufaransa, wamejizuia kuungana na mashabiki wengine kushuhudia michuano hiyo, badala yake wamebaki majumbani wakifanya ibada zaidi katika mwezi huu.


Comments