WACHEZAJI 8 WENGINE WALIOSTAAFU KUCHEZEA TIMU YA TAIFA MAPEMA


WACHEZAJI 8 WENGINE WALIOSTAAFU KUCHEZEA TIMU YA TAIFA MAPEMA

Kustaafu

Na Naseem Kajuna

Siku ya Jumapili baada ya kupoteza fainali ya Copa America Centenario Lionel Messi akiwa na miaka 29 pekee alitangaza kuachana na soka la kimataifa. Messi alifunga magoli 55 katika mechi 113 alizochezea Argentina na uamuzi wake huu ulishangaza wengi kwani Messi bado ana uwezo wa kuisaidia timu hii ya Argentina.

Lakini Messi si mchezaji wa kwanza maarufu kufanya maamuzi kama haya. Tutazame wachezaji wengine walioamua kuachana na soka la kimataifa kabla ya mda wao.

Gerd Muller 28

Kustaafu 1

Muller ambaye alikuwa anajulikana kwa jina linguine la Der Bomber, alifunga magoli 68 katika mechi 62 alizochezea nchi yake West Germany. Aliwasaidia West Germany kutwaa michuano miwili mfululizo ya Euro na Kombe la Dunia mwaka 1972 na mwaka 1974 akifunga kwenye fainali za michuano yote hiyo dhidi ya timu za Soviet Union (2) na Netherlands.

Muller alicheza kwenye kombe la dunia mara mbili tu mwaka 1970 na mwaka 1974 lakini bado alishikilia rekodi ya mfungaji bora zaidi kwenye michuano hiyo kwa miaka 32 akiwa na magoli 14 kabla ya Ronaldo de Lima kuivunja mwaka 2006 na Klose kuwazidi wote wawili mwaka 2014 kwa magoli 16. Klose pia alivunja rekodi ya magoli ya timu ya taifa ya Germany ya Gerd Muller  ila yeye alihitaji mechi 75 za ziada ili kukamilisha hilo.

Muller alistaafu mpira wa kimataifa mapema baada ya ushindi wa West Germany kwenye kombe la dunia la mwaka 1974 kwa sababu hakupenda kitendo cha wake wa wachezaji kutoruhusiwa kushiriki kwenye sherehe yao ya ubingwa baada ya mechi.

Alan Shearer 29

Kustaafu 2

Hakika nafasi ya 6 kwenye orodha ya wafungaji bora wa timu ya England haimtendei haki Alan Shearer. Mchezaji huyu aliichezea timu yake kwa mara ya kwanza akiwa na miaka 22 na wengi walidhani kwamba angekuwepo kwenye timu ya taifa kwa miaka mingi na angeweza kupata mafanikio yaleyale ya ajabu aliyoyapata kwenye mpira wa klabu.

Baada ya England kushindwa kufuzu kwa ajili ya Kombe la dunia la mwaka 1994 kulikuwa na presha kubwa kwa Shearer na wenzake kufanya  vizuri kwenye michuano ya Euro 1996 miaka miwili baadaye. Shearer alikuwa na presha zaidi juu yake  kwani alishindwa kufunga goli kwa ajili ya nchi yake tangu afunge mawili dhidi ya USA mwaka 1994.

Shearer alimaliza kama mfungaji bora wa michuano hiyo na magoli matano na akaongeza mengine mawili kwenye kombe la dunia la mwaka 1998 ambapo kwa wakati huo alikuwa kashapewa unahodha.

Lakini baada ya kupata majeraha kadhaa alitangaza kwamba Euro ya mwaka 2000 ndiyo itakuwa michuano yake ya mwisho kama mchezaji wa England. Licha ya kuitwa sana kwenye timu ya taifa mwaka 2002 na 2004 alimaliza kuichezea England akiwa amefunga magoli 30 katika mechi 63 pekee.

Paul Scholes 29

Kustaafu 3

Scholes hakuweza kuonesha uwezo wake wote kwenye timu ya  England ambayo alisema kwamba ilikuwa imejaa wachezaji wachoyo. Mchango wake unaokumbukwa akiwa amevaa jezi ya England ni kufunga goli katika mechi yake ya kwanza ya England na kufunga hat-trick ya kwanza ya England ndani ya miaka 6 mwaka 1999 dhidi ya Poland.

Muda wake kwenye timu ya England uliisha mapema baada ya Euro 2004 baada ya England kufungwa na Portugal kwa Penati. Scholes aliwekwa winga ili kuwezesha Frank Lampard na Steven Gerrard kucheza kama viungo wa kati. Alishindwa kucheza vizuri kwenye nafasi hiyo na alitolewa kwenye mechi yake ya mwisho. Alistaafu baada ya michuano hiyo.

Eric Cantona 28

cantona

Cantona ni gwiji mwingine wa timu ya Manchester United ambaye akuweza kucheza mpira wa kimataifa kwa mda mrefu. Baada ya kumpiga teke shabiki kwenye mechi ya Manchester United dhidi ya Crystal Palace mwaka 1995, muda wake kwenye timu ya Ufaransa ulikuwa umeisha.

Kifungo chake cha miezi nane kilipoisha, Cantona alijikuta akiwa amepoteza unahodha wa Ufaransa na alimkuta Zinedine Zidane akiwa amechukua nafasi yake kama mchezaji bora kwenye timu ya Ufaransa.

Licha ya Ufaransa kushindwa kufuzu kwa ajili ya kombe la Dunia la mwaka 1994, Cantona aliweza kufunga magoli 20 katika mechi 45 alizochezea  nchi yake.

Paul Breitner 22

Kustaafu 4

Breitner ni mmoja wa wachezaji wanaokumbukwa zaid kwenye timu ya Ujerumani. Der Afro kama alivyojulikana aliamua kustaafu mpira wa kimataifa mwaka 1975 akiwa na miaka 22 baada ya kufunga kwenye fainali ya kombe la dunia mwaka mmoja kabla.

Sababu aliyotoa ilikuwa ni ndoto yake ya kucheza klabu ya Real Madrid nchini Spain na mchezaji mwenzake kwenye timu ya Ujerumani Gunter Netzer

Lakini alirudi tena Ujerumani na akachezea nchi yake kwa mara nyingine tena lakini fikra zake za kisiasa zilimfanya akatae kucheza kombe la dunia la mwaka 1974 nchini Argentina kwa sababu ya ugaidi na ufisadi mkubwa uliokisiri nchini humo kwa wakati huo.

Samir Nasri 27

Kustaafu 5

Baada ya msimu wake mzuri na klabu ya Arsenal Nasri alitangazwa kuwa mchezaji bora wa Ufaransa mwaka 2010 lakini cha kushangaza ni kuwa hakuitwa kwenye timu yao ya kombe la dunia 2010 na alifanyiwa hivyohivyo tena mwaka 2014.

Nasri aliwashtaki wachezaji wenzake kwa kumsema nyuma ya mgongo wake kitu ambacho familia yake na ndugu zake pia waliamini. Baada ya mchumba wa Samir Nasri kumtukana kocha wa Ufaransa Deschamps, kocha huyu wa Ufaransa wa sasa alimfungulia mchumba wake Nasri mashtaka.

Tukio hili na mengineo kama haya yalimfanya Nasri kusema kuwa kila kitu kuhusu timu ya taifa kinamhuzunisha. Baada ya kukatwa kwenye kikosi  cha kombe la dunia mwaka 2014 nasri alistaafu mpira wa kimataifa milele.

Mwaka 2015 alisema kwamba hatochezea timu ya taifa ya Ufaransa hata kama baba yake akipewa ukocha wa timu hiyo.

Kevin Prince Boateng 24

Kustaafu 6

Boateng ni mmoja ya wachezaji wadogo zaidi kustaafu mpira wa kimataifa.Boateng aliamua kuhama kutoka kechezea timu za vijana za Ujerumani mpaka timu ya taifa ya Ghana kabla ya kombe la dunia la mwaka 2010 ambapo alikuwa kati ya wachezaji bora zaidi kwenye michuano hiyo.

Alistaafu mpira wa kimataifa kwa kutoa sababu za kiafya lakini aliitwa tena kwenye kikosi cha Black stars kwa ajili ya kombe la dunia la mwaka 2014.

Boateng alichezea nafasi yake ya pili kwenye timu hiyo baada ya kumtukana kocha wa Ghana James Appiah, kitu kilichomfanya arudishwe nyumbani kutoka kwenye kikosi cha Ghana. Boateng hakuondoka kwa heshima kwani aliutukana mpira mzima wa Ghana kwa kusema kwamba ni wa kishamba.

Carlos Roa 30

Kustaafu 7

Roa alionekana kuwa kwenye 'form' ya maisha yake baada ya kuweza kumaliza mechi zote za kufuzu kwa ajili ya kombe la dunia la mwaka 1998 bila kufungwa goli hata moja. Kwenye kombe la dunia la mwaka huo aliweza kuiasaida Argentina kumtoa England kwa kudaka Penati ya David Batty.

Mwaka mmoja baadae kipa huyu aliamua kustaafu mpira wa kimataifa na kwenda kwenye safari ya kidini na mke wake kwa sababu alikuwa anaamini mwisho wa dunia ulikuwa unakaribia.



Comments