SUAREZ AMKOROMEA KOCHA NA KUMALIZIA HASIRA ZAKE KWA KUPIGA NGUMI UZIO WA BENCHI URUGUAY IKIAGA COPA AMERICA ...kocha wake anena
Luis Suarez ameshindwa kuzuia hasira zake na kuishia kulipiga kwa ngumi benchi la wachezaji wa akiba katika mchezo wa Copa America dhidi ya Venezuela.
Hakuchezeshwa katika mchezo huo wa kipigo cha kuduwaza cha 1-0 na kupelekea Uruaguay kuaga michuano hiyo baada ya kufungwa pia 3-1 na Mexico katika mchezo wao wa kwanza.
Goli la Salomon Rondon la kipindi cha kwanza likatosha kuimaliza Uruguay huku karibu muda wote wa mchezo Suarez akiamini kuwa ataingizwa uwanjani kuikoa nchi yake.
Hata hivyo ilibainika baadae kuwa licha ya Suarez kupasha mwili moto na wenzake kabla ya mchezo, lakini jina lake halikuwepo hata kwenye wachezaji wa akiba.
Wakati mashabiki walipokuwa wakiimba jina lake kutaka aingizwe, Suarez ambaye hakucheza pia katika mchezo wa kwanza, aliinuka na kupasha mwili lakini kocha Oscar Tabarez alipoanza kufanya mabadiliko, mshambuliaji huyo hakuitwa.
Kwanza aliitwa aliingizwa Diego Rolan, baadae Nicolas Lodeiro na mwishowe Matias Corujo hatua iliyopekea Suarez kwenda kumkoromea kocha wake na kupiga uzio wa benchi.
Lakini hakukuwa na namna, Suarez asingeweza kucheza mchezo huo kwa kuwa jina lake halikujumuishwa kwenye orodha ya wachezaji wa akiba. Pengine hakufahamishwa hilo.
Kocha Tabarez akasema baada ya mchezo: "Suarez hayuko tayari kucheza, hiyo ni juu ya madaktari. Hata imkere kwa kiasu gani - na hakunieleza kitu chochote - sitamchezesha mchezaji ambaye hayuko fiti kwa asilimia 100".
Luis Suarez akipiga uzio wa benchi kwa hasira
Nyota wa Barcelona akiwa mnyonge kwenye benchi
Suarez alipasha mwili na wachezaji wenzake wa Uruguay kabla ya mchezo na Venezuela
Suarez, ambaye pia alikosa mchezo dhidi ya Mexico akipashwa mwili moto lakini hakuingizwa dimbani
Salomon Rondon akishangilia bao lake
Comments
Post a Comment