ROY HODGSON AMUHAKIKISHIA WAYNE ROONEY NAMBA KIKOSINI MWAKE



ROY HODGSON AMUHAKIKISHIA WAYNE ROONEY NAMBA KIKOSINI MWAKE
ROY Hodgson amemuhakikishia namba katika kikosi cha kwanza, Wayne Rooney katika fainali za Euro 2016.

Kocha huyo wa timu ya taifa ya England, alionyesha kukerwa na maswali kuhusu nahodha wake, akidai Rooney anaweza kucheza popote kwenye timu yake.

Rooney anatambulika kimataifa kama mmoja wa mastraika wakali, laini amekuwa akitumika zaidi katika nafasi tofauti katika miaka ya karibuni kwenye klabu yake na timu ya taifa.

Alimaliza msimu ulioisha akiwa kiungo wa Manchester United na akatumika namba 10 katika mechi ya kirafiki ya timu ya England dhidi ya Ureno Alhamisi.

"Sitaki hii iwe ni shoo ya Wayne Rooney," alisema kwa ukali alipoulizwa kama Rooney ana nafasi katika kikosi chake.


"Ni tatizo kuwa na mastraika wengi wakali. Sidhani kama tumeshakuwa na hali kama hii kwa muda mrefu," alisema.


Comments