ROBO FAINALI YA KWANZA EURO 2016, NI POLAND VS URENO…LEWANDOWKSKI VS RONALDO


ROBO FAINALI YA KWANZA EURO 2016, NI POLAND VS URENO…LEWANDOWKSKI VS RONALDO

Portugal vs Poland

Na Mahmoud Rajab

Poland na Ureno leo wanakutana katika mchezo wa robo fainali ya kwanza kabisa katika michuano ya Euro mwaka huu, mchezo utakaofanyika kunako dimba la Stade Vélodrome lililopo jijini Marseille.

Taarifa za kila timu.

Kiungo mahiri wa Poland Bartosz Kapustka leo anarejea baada ya kukoso mchezo dhidi ya Uswisi kutokana na kutumikia adhabu ya kadi mbili za njano.

Kipa namba moja wa Poland Wojciech Szczesny kwa mara nyingine tena hatakuwepo kutokana na kuendelea kuuguza jeraha lake la paja.

Ureno wana uwezekano mkubwa wa kuwa na viungo wao Raphael Guerreiro na Andre Gomes, ambao walikuwa wakiuguza majeraha yao madogo ya misuli.

William Carvalho, Pepe na Ricardo Quaresma  wote kwa pamoja wana kadi za njano na ikiwa leo watapata kadi nyingine na timu yao kufuzu hatua ya nusu fainali basi wataukosa mchezo huo.

Vivyo hivyo kwa upande wa Poland,  Kamil Grosicki, Artur Jedrzejczyk, Krzysztof Maczynski, Michal Pazdan, Slawomir Peszko, Lukasz Piszczek wote wana kadi za njano.

Taarifa muhimu za mchezo.

Baada ya kumwona Lionel Messi akiangukia pua tena katika mashindao mbalimbali ngazi ya timu ya taifa, Cristiano Ronaldo anafahamu fika kwamba kwa kufanya vizuri kwenye michuano hii, itakuwa tiketi tosha ya kumfanya kubeba Ballon d'Or na pengine kuwa mchezaji bora kabisa kuwahi kutokea katika kizazi cha sasa.

Kama Ureno watapoteza mchezo wao dhidi ya Poland, je, Ronaldo pia atatangaza kustaafu kama alivyofanya Messi baada ya Argentina kufungwa na Chile katika fainali ya Copa America wiki iliyopita?, sisi hatufahamu tunamwachia mwenyewe.

Akiwa na umri wa miaka 31, na hivyo taratibu kuanza kuingia utu uzima na kuuacha umri adhimu kwa mchezo wa soka, hii ni fursa kubwa kwake kuipa matokeo timu yake ambayo kwenye michuano ya safari hii imekuwa ikipenya kibahati-bahati.

Hata hivyo, kwa hatua waliyofika na timu zilizofuzu, Ureno ndio wanaonekana kupata timu rahisi kuliko nyingine. Hawajawahi kushinda mchezo wowote katika michunao hii kabla ya mwaka huu, lakini mpaka sasa wako pungufu ya mchezo mmoja kuifikia rekodi yao bora katika michuano mikubwa ngazi ya timu ya taifa (walifika nusu fainali kwenye Kombe la Dunia mwaka 1982).

Safu yao ya ulinzi imekuwa na imara kabisa licha ya kuruhusu goli dhidi ya Uswisi lilofugwa na Xherdan Shaqiri, goli lilofanya kuvunja rekoadi yao ya kutoruhusu goli tangu kuanza kwa mashindano. Hiyo imekuwa ni mara ya tatu kuruhusu goli tangu kuanza kwa mwaka 2016

Kikubwa wanachotakiwa kufanya ni kuhakikisha wanakuwa makini katika safu yao ya ushambuliaji. Mpaka sasa wamefunga magoli mawili tu, idadi ndogo zaidi kuliko timu yoyote katika hatua hii huku mshambuliaji nguli wa timu hiyo Robert Lewandowski akiwa hajaliona lango mpaka sasa. Ikumbukwe kuwa Lewandowski alifunga magoli 13 wakati wa michezo ya hatua ya awali ya kufuzu kuelekea michuno hii.

Takwmu za michezo waliyokutana.

  • Hii inakuwa ni mara ya tatu kati ya Poland na Ureno katika michuano mbalimbali. Poland walishinda 1-0 mwaka 1986 katika fainali za Kombe la Dunia na baadaye Ureno kushinda 4-0 katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2002.
  • Poland hawajapoteza dhidi ya Ureno katika michezo yao mitatu ya mwisho (wameshinda mara moja, wametoka sare mara mbili).
  • Mara ya mwisho kukutana, timu hizi zilitoka sare ya 0-0, mchezo uliofanyika Warsaw mwaka 2012.

Poland

  • Mara ya mwisho kufika hatua ya nusu fainali katika michuano mikubwa ilikuwa ni kwenye Kombe la Dunia mwaka 1982.
  • Mara ya mwisho Poland kushinda mchezo wa hatua ya mtoano (ukiondoa kwa njia ya mikwaju ya penati dhidi ya Uswisi) ilikuwa ni mwaka 1982 dhidi ya Ufaransa (walishinda 3-2).
  • Poland ndio iliyofunga magoli machache mpaka sasa, wamefunga magoli 3 katika michezo minne.
  • Tangu kuanza kwa michuno ya mwaka huu hawajawahi kuwa nyuma katika mchezo wowote. Wameruhusu goli moja tu mpaka sasa katika michezo minne.
  • Hajawahi kufunga goli zaidi ya moja katika mchezo mmoja katika michezo 10 ya Euro.
  • Jakub Blaszczykowski amehusika moja kwa moja katika magoli yote matano ya Poland katika michuano miwili ya Euro iliyopita (amefunga magoli 3 na kutoa pasi mbili za magoli).

Ureno

  • Ureno ndio timu pekee kufika hatua ya robo fainali kwenye kila michuano ya Ulaya tangu mwaka 1996.
  • Wana nafasi ya kufika nusu fainali kwa mara ya tano katika fainali saba za michuano hii.
  • Ureno ndio timu iliyocheza michezo mingi zaidi (32) katika historia ya michuano hii bila ya kushinda taji.
  • Hawajafungwa kwenye mechi 11 za ushindani chini ya kocha Fernando Santos (wameshinda mara 8, sare mara tatu). Ushindi wa mecho zote nane ulikuwa kwa tofauti ya goli moja (ukiwemo dhidi ya Croatia)
  • Ureno wamepata kadi chache zaidi katika michuano ya mwaka huu miongoni mwa timu zilizofika hatua hii (kadi tatu kwenye michezo minne)
  • Cristiano Ronaldo amecheza mechi nyingi zaidi ya mchezaji yoyote katika michuano hii. Amebakisha goli moja tu kufikia rekodi ya magoli nane ya Michel Platini aliyoweka katika michuano hii tangu mwaka 1984.
  • Ronaldo amefunga magoli 2 katika michezo 12 ya hatua ya mtoano katika michuano mbalimbali kwenye timu ya taifa.


Comments