RAIS WA ARGENTINA AMGONGEA SIMU LIONEL MESSI KUMUOMBA ASIIACHE TIMU YAKE



RAIS WA ARGENTINA AMGONGEA SIMU LIONEL MESSI KUMUOMBA ASIIACHE TIMU YAKE
RAIS wa Argentina, Mauricio Macri binafsi amenyanyua simu na kumpigia straika wa timu ya taifa hilo, Lionel Messi ili kujaribu kumshawishi staa huyo wa Barcelona asistaafu kuchezea timu hiyo ya taifa.

Jumapili iliyopita Argentina walifungwa na Chile kwa mikwaju ya penati katika mechi ya fainali ya michuano ya Kombe la Copa America na baada ya Messi kukosa penati alibubujikwa na machozi na kisha baada ya mechi akadai kuwa kazi yake ya kuitumikia timu hiyo imemalizika.

Hata hivyo, msemaji wa rais wa Argentina jana aliliambia shirika la habari la Ufaransa (AFP) kwamba rais Macri alimpigia simu na kumweleza jinsi anavyojivunia kiwango vcha timu ya taifa na akamshauri kutosikiliza lawama za watu.

"Rais Macri alimpigia simu na kumweleza jinsi anavyojivunia kiwango kinachoonyeshwa na timu ya taifa na akamtaka kutosikiliza lawama za watu," alisema msemaji huyo.

Mbali na kumpigia simu, msemaji huyo alisema kuwa pia rais Macri vilevile alimtumia ujumbe Messi wa kumuunga mkono kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter.

"Sijawahi kujisikia vibaya kwa kiwango cha timu yetu ya taifa," alieleza rais huyo kupitia katika ujumbe huo.

"Nina matumaini furaha yetu ya mafanikio itaendelea kwa miaka mingi zaidi," aliongeza.


Comments