KIUNGO wa Ufaransa na Juventus anayehusishwa na usajili wa kurejea Manchester United, Paul Pobga amesema hajutii kitendo chake alichokifanya mwaka 2012 cha kumwambia Alex Ferguson kuwa anataka kuondoka Old Trafford.
Akizungumza kwenye kambi ya Ufaransa inajiandaa na Euro 2016, Pobga alisema: "Ni kocha ninayemheshimu sana. Lakini yeye ni binaadamu. Mimi huwa sisiti kusema kile ninachokifiria. Iwe ni Ferguson au Barack Obama nitasema tu.
"Ferguson alinifuata, tukazungumza. Alitaka nibaki United, lakini tayari nilikuwa na maamuzi yangu."
Pobga anatajwa kuwaniwa na Manchester United kwa pauni milioni 78.
Pogba alisaini Juventus baada ya kuondoka United na kufanikiwa kushinda mataji mengi Italy
Pogba (katikati) aliondoka United mwaka 2012 akiwa amecheza mechi tatu za kikosi cha kwanza
Comments
Post a Comment