PEP Guardiola na Jose Mourinho wanaaminika kuvutiwa na straika wa Borussia Dortmund, Pierre-Emerick Aubameyang, wakati Manchester City ikijiaminisha kwamba Lionel Messi atachagua kuchezea timu hiyo badala ya Manchester United.
Kwa kuwa Aubameyang anatarajiwa kugharimu euro milioni 80, utakuwa uhamisho wa rekodi Uingereza kama supastaa huyo raia wa Gabon ataondoka Ujerumani na kwenda England.
Real Madrid pia inaripotiwa kudhamiria kumtia mikononi straika huyo.
"Makocha wapya wa United na City wote wanamtaka straika wa Borussia Dortmund. Vinginevyo kama kuna uhamisho kwa Real Madrid, lakini klabu za Manchester zimejipanga kupambana kwa ajili ya mwanasoka huyo bora wa mwaka Ujerumani," limeripotia gazeti la Daily Star la Uingereza.
Makocha hao wa zamani wa Barcelona na Real Madrid pia wanaweza kuingia vitani kwa ajili ya Messi.
Baada ya taarifa za United kuonyesha nia ya kumtaka staa huyo raia wa Argentina wiki iliyopita, gazeti la The Manchester Evening News limeripoti kwamba Mtendaji Mkuu wa City, Ferran Soriano anaamini kuwa Etihad itakuwa chaguo la kwanza kwa Messi kama ataondoka Barcelona.
Comments
Post a Comment