PELE ASEMA NEYMAR BADO SANA KWA RONALDO NA MESSI


PELE ASEMA NEYMAR BADO SANA KWA RONALDO NA MESSI


EDSON Arantes do Nascimento aliye maarufu kwa jila la Pele, anayedhaniwa kuwa mwanasoka bora wa dunia wa muda wote,  ameliambia gazeti la MARCA la Hispania kuwa Neymar haufikii ubora waliokuwa nao Cristiano Ronaldo na Lionel Messi.

Mkongwe huyo wa miaka 75 aliyasema hayo akiwa barani Ulaya kupigia debe ujio wa filamu inayozungumzia maisha yake inayokwenda kwa jina la 'Pele: Birth of a Legend'.

"Nimekuwa nikimjua Neymar tangu alipokuwa mdogo na miaka mingi iliyopita makocha wake waliniambia kuwa alikuwa vizuri sana. Ni hivyo lakini hana ubora wa Ronaldo au Messi.

"Kama ningalipaswa kusema ni nani mchezaji namba moja leo, ningalisema Lionel. Mreno (Ronaldo) ana staili yofauti ya uchezaji lakini kwa maoni yangu aliye bora ni Messi," alisema Pele.


Comments