PELE AMSHUSHA KIWANGO NEYMAR MBELE YA MESSI, RONALDO



PELE AMSHUSHA KIWANGO NEYMAR MBELE YA MESSI, RONALDO
MWANASOKA wa zamani, Abeid Pele amemponda straika wa Barcelona, Neymar akisema kuwa licha ya kusadikiwa kuwa ana kiwango kikubwa lakini hawezi kuwafikia Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

Kiwango cha Neymar kinasemekana kuongeza makali katika safu ya ushambuliaji Barcelona ambayo imepachikwa jina la "MSN" akiwa na mshindi mara tano wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia ballon d'Or, Messi na Luis Suarez.

Staa huyo mwenye umri wa miaka 24 ambaye msimu uliopita alifunga mabao 31 katika mashindano yote, alishika nafasi ya tatu nyuma ya Messi na Ronaldo katika kinyang'anyiro hicho cha ballon baada ya kuisaidia Barca kutwaa mataji matatu msimu wa 2014/15.

Hata hivyo raia mwenzake huyo, Pele ambaye ni mchezaji bora wa muda wote anasema kuwa Neymar hayuko katika ubora walionao Messi na Ronaldo.

"Namfahamu Neymar tangu akiwa mdogo na kwa miaka mingi makocha wake wamekuwa wakiniambia ni mchezaji mzuri," Pele aliliambia gazeti la Marca.

"Hili linawezekana lakini hana kiwango kinachowafikia Ronaldo ama Messi."


"Endapo nitaulizwa kwa leo ni mchezaji yupi namba moja, nitasema ni Leonel. Kwa upande wake ana staili ya uchezaji wake, mawazoni mwangu mchezaji ni Messi," alisema nyota huyo wa zamani.


Comments