PATRICE EVRA AWAONYA PAUL POGBA NA ANTOINE GRIEZMANN



PATRICE EVRA AWAONYA PAUL POGBA NA ANTOINE GRIEZMANN
BEKI mkongwe Patrice Evra amewaonya wachezaji wenzake katika timu ya taifa ya Ufaransa, Paul Pogba na Antoine Griezmann kukubali kubeba lawama endapo watashindwa kufanya vizuri katika michuano ya fainali za mataifa ya Ulaya "Euro 2016" zinazonza kufanyika leo.

Kuandaliwa kwa mashindano hayo nchini Ufaransa kunatajwa kuwa ni bahati ya kurudia mafanikio ya mwaka 1998 wakati walipotwaa Kombe la Dunia na sasa kiungo huyo wa Juventus, Pogba na wa Atletico Madrid, Griezmann wanatakiwa kufanya hivyo.

Griezmann anatwishwa mzigo huo kutokana na kukosekana Karim Benzema, lakini Evra anaamini kukosekana kwa nyota huyo wa Real Madrid kutawatia presha kwa waliobaki.

"Ni rahisi kusema ni vigumu lakini watu wanatarajia mengi kutoka kwao," Evra aliuambia mtandao wa Journal du Dimanche.

"Ninawatahadharisha; Karim hatuko nae na kila kitu kitakwenda vibaya watanyooshewa vidole," aliongeza nyota huyo.


Comments