Kiungo mkabaji wa Chelsea Nemanja Matic amemwambia bosi mpya wa klabu hiyo Antonio Conte kuwa anataka kwenda Manchester United kuungana na Jose Mourinho, hiyo ni kwa mujibu wa The Sun la Uingereza.
Jose alimrejesha Stamford Bridge nyota huyo wa Serbia wakati aliopenda kuifundisha Chelsea kwa maea ya pili na sasa ana matumaini makubwa ya kumsajili kiangazi hiki.
Licha kuwa moja ya wachezaji muhimu waliochangia ubingwa wa Chelsea msimu wa 2015, Matic akaibuka kuwa 'mzigo' msimu uliofuata wakati Mourinho alipotimuliwa.
Inadaiwa wawili hao walizinguana wakati Mourinho alipomtoa Matic dakika 27 tu baada ya kuingia uwanjani kwenye kipigo cha bao 3-1 kutoka kwa Southampton, lakini hali halisi ni kwamba kocha huyo ni shabiki mkubwa wa kiungo huyo.
Matic ni mmoja wa wachezaji wachache wa Chelsea walioongea na kuonyesha kukerwa kwao baada ya Mourinho kutimuliwa.
Comments
Post a Comment