MWAKA WA TABU NIGERIA …BAADA YA KESHI, KOCHA MWINGINE WA TIMU YA TAIFA AFARIKI DUNIA



MWAKA WA TABU NIGERIA …BAADA YA KESHI, KOCHA MWINGINE WA TIMU YA TAIFA AFARIKI DUNIA

Wakati Nigeria bado inaomboleza kifo cha mchezaji na kocha wao wa zamani Stephen Keshi aliyeaga dunia wiki iliyopita, taifa hilo limepata pigo lingine kwa kufiwa na kocha mwingine za wa zamani wa timu ya taifa.

Shirikisho la soka la Nigeria linasema kuwa mkurugenzi wa kiufundi ambaye pia alikuwa kocha wa zamani wa timu ya taifa Amodu Shuaibu, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 58.

Bwana Shuaibu (pichani juu), kocha mara nne wa timu ya Super Eagles alianza kuumwa na kifua Ijumaa usiku na baadaye akaaga duniani akiwa usingizini.


Comments