MIRAELM PJANIC AZIACHA SOLEMBA CHELSEA NA MAN UNITED


MIRAELM PJANIC AZIACHA SOLEMBA CHELSEA NA MAN UNITED

MIRAELM Pjanic amekamilisha usajili wake kutoka Roma na kujiunga na Juventus, hivyo kuziacha solemba Chelsea na Manchester United zilizokuwa zikimtolea macho.

Kocha ajaye Chelsea, Antonio Conte aliripotiwa kunuia kumpeleka kiungo huyo Stamford Bridge sambamba na mchezaji mwenzake Radja Nainggolan, huku Jose Mourinho naye akielezwa kumfanya Mbosnia huyo wa miaka 20 kuwa moja ya malengo yake Old Trafford.

Pjanic aliwasili Turin kufanyiwa vipimo vya afya mapema Jumatatu, kisha akajiunga na klabu hiyo kwa dau la pauni milioni 25 akisaini mkataba wa miaka mitano.


Comments