MANCHESTER United imeweka mezani ofa ya pauni milioni 35.2 kwa ajili ya kumsajili kiungo wa kati wa Valencia, Andre Gomes katika dirisha la usajili wa kiangazi hiki.
Gomes alifunga mabao tisa katika mechi 77 alizoichezea Valencia tangu alipoichezea kwa mara ya kwanza timu hiyo ya La Liga mwaka 2014, lakini staa huyo wa miaka 22 sasa anahusishwa kwa nguvu na kuhamia Old Trafford.
Mwandishi wa habari wa Italia anayesifika kwa kuandika habari zenye ukweli, Alfredo Pedulla ameripoti kuwa United imeweka mezani pauni milioni 35.2 kwa ajili ya Mreno huyo, pamoja na bonasi ya pauni milioni 11.7.
Jose Mourinho yupo katika harakati za kuiongezea nguvu safu ya kiungo ya United baada ya kukabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo mwishoni mwa Mei.
Inaeleweka kuwa mwakilishi wa Gomes, Jorge Mendes ambaye pia ni wakala wa Mourinho atasaidia kusukuma mchakato wa kufanikisha dili hilo.
Comments
Post a Comment