KAMPENI za kusaka saini ya kiungo wa Juventus Paul Pobga zinazidi kupamba moto ambapo sasa inaelezwa Manchester United ipo tayari kuwapa mabingwa hao wa Italia beki Matteo Darmian.
Beki huyo wa pembeni atatolewa kama chambo cha kuongeza ushawishi kwa Juventus ili United ifanikishe safari yake ya kumrejesha Paul Pogba Old Trafford.
Jose Mourinho amepania kumnasa kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa na inaaminika wiki iliyopita alipeleka ofa ya pauni milioni 60 lakini ikakataliwa na Juventus.
United sasa inatarajiwa kuongeza uzito kwa kumtoa Darmin, beki wa kimataifa wa Italia mwenye umri wa miaka 26 ambaye walimnunua kwa pauni milioni 12 kiangazi kilichopita kutoka Torino.
Comments
Post a Comment