MANCHESTER CITY imejitoa katika mbio za kumuwania kiungo wa Juventus, Paul Pogba hivyo kutoa nafasi kwa Manchester United kumrejesha kundini staa huyo raia wa Ufaransa.
Kwa mujibu wa gazeti la Manchester Evening News, kocha mpya wa City, Pep Guardiola ameliondoa jina la kiungo huyo katika orodha yake ya wachezaji anaowataka katika dirisha hili la usajili wa kiangazi.
Kutokana na ripoti hiyo, sasa Jose Mourinho anaweza kuweka mezani dau rekodi kwa England kwa ajili ya staa huyo wa miaka 23 katika harakati zake za kusuka kikosi kitakachompa taji la Premier League katika msimu wake wa kwanza Old Trafford.
Pogba amekuwa akihusishwa na uhamisho wa pauni milioni 60 kurudi katika klabu yake ya zamani, aliyoondoka mwaka 2012 baada ya kukosa uwezekano wa kucheza kikosi cha kwanza.
Comments
Post a Comment