Luiz Felipe Scolari anataka kuwa kocha mpya wa England, nafasi ambayo aliikataa miaka kumi iliyopita.
Scolari, 67, alikataa kuwa mrithi wa Sven Goran Eriksson mwaka 2006 baada ya FA kuweka hadharani utashi wao huo huku akiwa bado yupo kwenye mkataba wa kuifundisha Ureno.
Lakini baada ya Gareth Southgate kuweka wazi kuwa hana mpango wa kumrithi Roy Hodgson katika mkataba wa kudumu na kwamba anachoweza kufanya ni kuwa kocha wa muda tu, Scolari ameibuka na kusemma anaitaka nafasi hiyo.
Scolari, ambaye kwa sasa anafanya kazi China, ameiambia Daily Mail la Uingereza: "Kwasasa mimi ni kocha wa Guangzhou na ninaizingatia kazi yangu hapa. Lakini najua umuhimu wa kibarua cha England katika ulimwengu wa soka.
"Najua umuhimu wa kuwa kocha wa taifa kupitia muda wangu niliokuwa mwalimu wa Brazil na Ureno."
Comments
Post a Comment