LIVERPOOL NAYO YAMPIGIA HESABU JAMIE VARDY



LIVERPOOL NAYO YAMPIGIA HESABU JAMIE VARDY

LIVERPOOL itaamua wakati wa mashindano ya Euro 2016 iwapo itaamua kuingia kwenye mbio za kusaka saini ya mshambuliaji Jamie Vardy wa Leicester ambaye anawaniwa na Arsenal.
Klabu ya Arsenal imeweka wazi kuwa itatoa pauni milioni 20 ili kufikia kipengele cha manunuzi cha mchezaji huyo bora wa mwaka.
Lakini Daily Star linaandika kuwa Liverpool imekuwa ikimfuatilia Vardy, 29 kwa misimu miwili na sasa wataangalia ushiriki wake katika Euro 2016 kabla ya kuingia vitani.




Comments