Mtu mwenye jina kubwa katika soka la Nigeria, mmoja wa manahodha bora waliowahi kutokea, beki bora kabisa Afrika na kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria "Super Eagles"Stephen Okechukwu Keshi (pichani) amefariki kwa shambulio la moyo akiwa na umri wa miaka 54.
Emmanuel Ado, kaka wa marehemu amesema Keshi amefariki mapema leo Jumatanp, Juni 8.
"Kwa mapenzi yake Mungu, familia ya Ogbuenyi Fredrick Keshi inatangaza kifo cha Mr. Stephen Okechukwu Chinedu Keshi," ilisema taarifa hiyo ya Ado.
Taarifa hiyo ikaendelea: "Mtoto wetu, kaka yetu, baba yetu, mkwe wetu, shemeji yetu, amekwenda kuungana na mkewe (Nkemu) Bi Kate Keshi aliyefariki akiwa na umri wa miaka 35 Disemba 9, 2015.
"Tangu mkewe alipofariki, Keshi alikuwa kwenye maombolezo. Alirejea Nigeria kuwa naye. Alipanga kuondoka leo kurejea Marekani, kabla hajapata matatizo ya moyo na kufariki."
Mke wa Keshi alifariki kwa ugonjwa wa kansa.
Keshi aliyewahi kutwaa tuzo ya kocha bora Afrika, aliwahi pia kuwa kocha wa timu ya taifa ya Togo.
Comments
Post a Comment