KOCHA ARSENE WENGER AMFAGILIA N'GOLO KANTE... asema daima yupo anapotakiwa kuwa na anafanya anachopaswa kufanya



KOCHA ARSENE WENGER AMFAGILIA N'GOLO KANTE... asema daima yupo anapotakiwa kuwa na anafanya anachopaswa kufanya
ANATISHA, hivyo ndivyo unavyoweza kuitafsiri kauli ya kocha arsenal Wenger wakati akimmwagia sifa tele N'Golo Kante kama mchezaji shupavu, mahiri na wa kipekee ambaye anamkubali sana.

Kiungo huyo wa Leicester City alifanya maajabu katika msimu wake wa kwanza Ligi Kuu Uingereza, akiisaidia timu yake ambayo ilikuwa haipewi nafasi kubwa kutwaa ubingwa, klabu nyingi zimeonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Mtandao wa The Goal unaeleza kuwa unafahamu kwamba Arsenal wamefanya mazungumzo na nyota mwingine wa Leicester City, Jamie Vardy baada ya kuwa tayari kutoa pauni mil 20 kununua mkataba wake na Wenger amebainisha sasa kuwa yeye ni shabiki mkubwa wa Kante.

"Ninamkubali sana na ninampenda N'Golo Kante, ana mbinu tele," wenger aliliambia beIN Sports.

"Ni mchezaji wa kipekee sana kwa soka la Ulaya. Ana ubora wa aina yake, ana hisia za soka, ni watu wachache sana wanaoweza kuwa kama yeye. Daima yupo anapotakiwa kuwa na anafanya anachopaswa kufanya."

"Ni nadra sana kuwa na kiungo wa kati kama yeye. Si kwa upande wa kushoto tu lakini hata kulia pia."


Kante ametajwa kwenye tetesi za kuwa kwenye rada za Paris Saint-Germain na kwa sasa yupo kwenye kikosi cha Ufaransa kinachoshiriki Euro.   


Comments