REAL Madrid imeambiwa wazi na Juventus kwamba italazimka kulipa euro milioni 120 pamoja na kumwachia kungo wake Toni Kroos kama inataka kumchukua Paul Pogba.
Juventus imeripotiwa kuweka sharti hilo kama kigingi kwa Madrid kwa kuwa hawataki kumuuza staa wao kwa klabu hiyo ya Santiago Bernabeu.
Hata hivyo kama kiungo huyo Mfaransa atalazimika kuondoka, Juve wanamtazama Kroos kama mbadala sahihi wakiamini kuwa Mjerumani huyo ana vitu vingi vinavyomfanya kufanana na Pogba dimbani.
Comments
Post a Comment