JOSE MOURINHO AMTAKA LIONEL MESSI OLD TRAFFORD



JOSE MOURINHO AMTAKA LIONEL MESSI OLD TRAFFORD
MANCHESTER United wanaandaa uwezekano wa kufanya uhamisho mkubwa wa kumsajili straika wa Barcelona, Lionel Messi.

Gazeti la Daily Mail la Uingereza limeripoti kuwa, United imetuma maombi mara mbili katika wiki tatu zilizopita katika jaribio la kumsajili Muargentina huyo.

Uhamisho wowote unaonekana kulenga kuirejesha United katika Ligi ya Mabingwa Ulaya chini ya Jose Mourinho msimu wa 2017/18.

Usajili wa Messi unaweza kuvunja rekodi ya pauni mil 85.3 ambazo Real Madrid walilipa kwa Tottenham ili kumnasa Gareth Bale.
Mkataba wa sasa wa Messi Nou Camp unatarajiwa kumalizika 2018 na imebainika kuwa anahitaji kuhakikishiwa mambo kadha kama wanataka kumbakisha Barcelona ambapo amefunga jumla ya mabao 453 katika mechi 531.

United imekuwa ikisaka mchezaji mwenye jina kubwa na ishajaribu kumsajili Cristiano Ronaldo hivi karibuni, wakati pia ishajaribu kuwanasa Bale na Neymar mwaka jana.


Comments