Beki wa England John Stones amekataa mpango wa kwenda Barcelona — na sasa inaaminika anataka kwenda kwa Pep Guardiola huko Manchester City.
Barcelona ilikutana na wakala wa beki huyo - Paul Martin
wiki iliyopita juu ya ofa itakayompatia mshahara wa pauni 90,000 kwa wiki pamoja na marupurupu kibao, lakini ofa hiyo ikapigwa chini.
Barca imekuwa ikimfuatilia Stones tangu mwaka 2014 na licha ya kushuka kiwango kwa beki huyo mwishoni mwa msimu uliopita, lakini mabingwa hao wa Hispania bado wanaamini Stones ni chaguo sahihi.
Beki wa England na Everton John Stones amekataa mpango wa kwenda Barcelona
Stones (wa pili kushoto) akiwa na kikosi cha England kuelekea Euro 2016
Kocha wa Manchester City Pep Guardiola yuko katika nafasi nzuri ya kumnasa Stones
Comments
Post a Comment