HODGSON AWAAMBIA HARRY KANE NA RAHEEM STERLING SASA BENCHI LINAWAHUSU



HODGSON AWAAMBIA HARRY KANE NA RAHEEM STERLING SASA BENCHI LINAWAHUSU
England's Daniel            Sturridge, center, is mobbed by his teammates after scoring            his side¿s second goal during the Euro 2016 Group B soccer            match between England...
KOCHA wa England Roy Hodgson amewaambia Harry Kane na Raheem Sterling kuwa wamepoteza nafasi zao wenyewe na sasa wajiandae kukaa benchi Jumatatu katika mchezo wa Euro 2016 dhidi ya Slovakia siku ya Jumatatu.
Bosi huyo wa England aliwapumzisha washambuliaji hao kipindi cha pili kwenye mchezo dhidi ya Wales wakati wakiwa nyuma kwa bao la Gareth Bale lakini waliongia kuchukua nafasi zao - Jamie Vardy na Daniel Sturridge - wakaokoa jahazi kwa kufunga bao la kusawazisha na la ushindi.
Sasa Kane na Sterling watapaswa kusubiri wakati mwingine katika kipindi hiki ambacho kocha  Hodgson  amepania kufanya makubwa ili kujihakikishia tiketi ya kwenda hatua ya mtoano. 
Hodgson alisema: "Wachezaji wanapaswa kuthibitisha thamani yao, wakati mwingine mchezaji uliyemtegemea zaidi kabla ya michuano ndiye huyo huyo anayekuangusha.
"Wale uliokuwa umewaweka kwaajili ya kuwasaidia wale chaguo la kwanza, ndiyo wanaibuka kuwa bora zaidi."



Comments