FRANCESCO Totti atacheza msimu wake wa 25 – ambao ni wa mwisho katika kikosi cha Roma baada ya kusaini dili jipya la mwaka mmoja na klabu hiyo ya Serie A.
Starika huyo ambaye atagota miaka 40 Septemba mwaka huu, alihusishwa na uhamisho wa kushangaza kujiunga na mabingwa wa Premier League, Leicester City mwezi Machi, lakini badala yake amechagua kumalizia soka yake Roma.
"Kwa kweli niliutaka mkataba huu, unawakilisha kutambuliwa kwa ndoto yangu," Totti aliiambia tovuti ya klabu. "Mara zote nilitaka kumaliza kazi yangu mnikiwa nimevaa jezi moja tu ya Roma."
Totti alijiunga na timu hiyo ya Italia wakati akiwa na umri wa miaka 12 na miaka minne baadaye alicheza kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza, na tangu wakati huo amecheza mechi 758 na kufunga mabao 304 – ikiwa ni rekodi kwa klabu hiyo.
Comments
Post a Comment