EURO 2016: WENYEJI UFARANSA WAITANDIKA ROMANIA 2-1 ...bao la Dimitri Payet laiteka 'show'



EURO 2016: WENYEJI UFARANSA WAITANDIKA ROMANIA 2-1 ...bao la Dimitri Payet laiteka 'show'
Dimitri Payet shows his sheer joy after scoring the            winning goal in the 89th minute to hand his country a crucial            win
Wenyeji wa michuano ya ubingwa wa Ulaya (Euro 2016), Ufaransa wameanza vema kwa kuichapa Romania 2-1, lakini ni bao la Dimitri Payet ndilo lililouteka mchezo.

Dakika ya 89 wakati mchezo ukielekea kumalizika kwa sare ya 1-1, nyota huyo wa West Ham akaachia mkwaju wa mbali nje ya 18 uliokwenda moja kwa moja wavuni kupitia kona ya juu kushoto mwa lango la Romania.

Hakuna shaka kuwa goli hilo tamu litaangia moja kwa moja kwenye kinyang'anyiro cha magoli bora ya michuano hii iliyoanza kutimua vumbi Ijumaa usiku.

Ufaransa ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata goli la kuongoza kupitia kwa Olivier Giroud dakika ya 57 lakini Stancu akaisawazishia Romania kwa penalti tata kunako dakika ya 65.

Kwa kiasi kikubwa Ufaransa haikucheza vizuri lakini mabadiliko ya kumtoa Griezmann dakika ya 66 na nafasi yake kuchukuliwa na Coman pamoja na yale ya dakika ya 77 ya kumtoa Pobga na kumwingiza Martial, ndiyo yaliyoleta uhai kwa wenyejie.

UFARANSA (4-3-3): Lloris; Sagna, Rami, Koscielny, Evra; Pogba (Martial 77), Kante, Matuidi; Griezmann (Coman 66), Giroud, Payet (Sissoko 90+2)

ROMANIA (4-3-3): Tatarusanu; Sapunaru, Grigore, Chiriches, Rat; Stanciu (Chipciu 72), Hoban, Pintilii; Popa (Torje 82), Andone (Alibec 61), Stancu

Payet's strike heads towards                  the back of the net to win the game for the Euro 2016                  hosts at the Stade de France
Payet akiifungia Ufaransa bao la ushindi kwa mkwaju wa mbali kwenye uwanja Stade de France
Olivier Giroud wheels away                  in celebration after scoring the opening goal of this                  year's European Championship in France
Olivier Giroud akishangilia bao la kwanza la Ufaransa


Comments