URENO imeanza vibaya kampeni zake za kusaka taji la Euro 2016 baada ya kulazimishwa sare na timu isiyopewa nafasi - Iceland.
Luis Nani aliifungia Ureno bao la kuongoza dakika ya 31 lakini Bjarnason akaisawazishia Iceland dakika ya 50 wakati supastaa wa Ureno Cristiano Ronaldo akipoteza nafasi ya wazi ya kuifungia nchi yake bao la ushindi.
Ukingoni mwa mchezo, Nani alimtumia Ronaldo krosi tamu akiwa ndani ya sita lakini Ronaldo ambaye anaweza kuwa ndiye mfungaji bora wa magoli ya vichwa barani Ulaya, akaishia kupiga mpira uliokwenda mikononi mwa kipa Hannes Halldorsson.
Katika mchezo mwingine Austria ikachapwa 2-0 na Hungary kwa magoli yaliyofungwa na Adam Szalai na Zoltan Stieber.
Nani akishangilia goli lake
Nani akipiga mpira uliokwenda wavuni
Vieirinha anaserereka chini baada ya kuukosa mpira na kuruhusu Bjarnason wa Iceland afunge kirahisi
Bjarnason akiruka juu na kushangilia goli la kwanza kwa Iceland katika historia ya michuano ya Ulaya
Comments
Post a Comment