KOCHA wa timu ya taifa ya Hispania, Vicente del Bosque hana hakika nani kati ya David de Gea na Iker Casillas ataanza katika kikosi chake kitakachocheza mechi ya ufunguzi wa Euro 2016.
De Gea na nahodha Casillas wanapigania namba katika kikosi cha kwanza kwenye michuano hiyo ya mataifa ya Ulaya, ambako Hispania itawakabili Jamhuri ya Czech, Uturuki na Croatia.
Kikosi cha Del Bosque kilikamilisha maandalizi ya kuelekea Euro kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Georgia juzi usiku.
Akizungumza kuelekea mechi ya juzi, kocha huyo mwenye umri wa miaka 65, alisema hajafikia maamuzi ni kipa gani chagua la kwanza hadi kabla ya mechi yao ya ufunguzi Juni 13.
"Inawezekana kwamba De Gea atacheza (mechi ya juzi usiku). Casillas alicheza dhidi ya Korea Kusini na hicho tu ndicho ninachoweza kusema," Del Bosque alisema.
"Sihitaji kufanya maamuzi hayo sasa, nitaamua siku za baadae."
Licha ya kuifunga Korea Kusini 6-1 katika mechi iliyopita ya kirafiki, Del Bosque amekataa kuichukulia kiwepesi mechi yao ya ufunguzi wa Euro akisema hana hamna mechi nepesi.
Comments
Post a Comment