DAVID DE GEA amekumbwa na kashfa ya ngono iliyotishia kutimuliwa kwenye timu ya taifa ya Hispania inayoshiriki michuano ya Euro 2016.
Kipa huyo wa Manchester United jina lake limetajwa mahakamani na shahidi aliyedai kuwa De Gea alishiriki mahusiano na changudoa bila ridhaa yake.
Hata hivyo De Gea amekanusha vikali na kusema jambo hilo linashughulikiwa na mawakili wake.
De Gea amesema katika mkutano na waandishi wa habari: "Yote ni uongo. Najisikia mwenye nguvu zaidi kubakia timu ya taifa... habari hizo si za kweli na ipo mikononi mwa wanasheria wangu.
"Sikuwahi kufikiria suala la kuondoka timu ya taifa. Inanipa ari ya kufanya mazoezi kwa nguvu zaidi".
Tuhuma hizo zinasema mwaka 2012 kipa huyo namba moja wa United aliandaa mipango ya 'mechi' hiyo ya ngono kwaajili ya mchezaji mwenzake wa U-21 ya Hispania Iker Muniain pamoja na mchezaji mwingine ambaye hakutajwa jina dhidi ya changudoa bila ridhaa yake.
Tovuti moja ya Hispania El Diario inasema madai hayo yalikuwa sehemu ya ushahidi uliotolewa kwa waendesha mashtaka katika kesi ya mfanyabishara wa danguro la ngono Torbe ambaye jina lake halisi ni Ignacio Allende Fernandez.
Torbe alibakia rumande mwezi April baada ya kukutwa na hatia ya kuendesha biashara ya ukahaba kwa kutumia wasichana wenye umri mdogo.
Shahidi aliyetambulika kama TP3 akadai De Gea aliandaa mkutano na Torbe kwa niaba ya Muniain na mchezaji mwingine katika hotel ya nyota tano jijini Madrid mwaka 2012.
Mpelelezi wa Kihispania ameripotiwa akisema anaamini katika ushahidi uliotolewa na TP3 pamoja na wanawake wengine wawili waliohojiwa katika utaalamu wa hali ya juu.
Ripoti ya polisi iliyotolewa Juni 3, 2015 ilisema: "Baada ya kumwacha mwanamke huyo chumbani pamoja na msichana mwingine, Torbe alimwambia wanapaswa kulalala na wanasoka na kukubali kufanya kila watakalotaka na kwamba hatua hiyo ingewaingizia kipato kikubwa.
Comments
Post a Comment