TIMU ya Juventus imempokea kwa mikono miwili staa Dani Alves, baada ya beki huyo wa zamani wa Barcelona kuwasili mjini Turin akitokea mapumzikoni nchini Brazil.
Kinara huyo mwenye umri wa miaka 33 alikubali kujiunga na mabingwa hao wa Italia mapema mwezi huu, lakini hadi sasa alikuwa bado na timu ya taifa ya Brazil iliyokuwa ikishiriki fainali za Copa America.
Wakati akiwasili mjini humo, Alves alikuwa ameambatana na wakala wake na alisaini mkataba baada ya kufuzu vipimo vya afya.
Baada ya kumaliza mchakato huo, klabu hiyo ilituma ujumbe wa kumkaribisha ulioambatana na picha za kuwasili kwake.
Comments
Post a Comment