DANI ALVES AMSHAURI PHILIPPE COUTINHO KUITEMA LIVERPOOL



DANI ALVES AMSHAURI PHILIPPE COUTINHO KUITEMA LIVERPOOL
BEKI wa timu ya taifa ya Brazil, Dani Alves amemshauri Mbrazil mwenzake, Philippe Coutinho kufikiria kuitema Liverpool.

Coutinho, 23, amekuwa chachu katika safu ya kungo ya Liverpool tangu alipowasili kwa ada ya pauni mil 8.5 akitokea Inter Milan januari 2013.

Kutokana na kipaji chake, ameshafunga mabao 12 katika mechi 43 yaliyomfanya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Liverpool ukiwa ni msimu wake wa pili mfululizo.

Kutokana na hali hiyo, Alves ambaye juzi alicheza na Coutinho katika mechi yao ya kwanza ya michuano ya Kombe la Copa Amerika dhidi ya Ecuador, alimpongeza staa huyo na akasema ana kiwango cha kucheza kwenye klabu ya Nou Camp.


"Soka ni kitu cha kuwa na kumbukumbu katika historia na hivyo natakiwa kufikiria kuchezea klabu kubwa zaidi," alisema staa huyo.


Comments