CRISTIANO RONALDO AMMWAGIA SIFA WAYNE ROONEY



CRISTIANO RONALDO AMMWAGIA SIFA WAYNE ROONEY
STRAIKA wa timu ya taifa ya Ureno, Cristiano Ronaldo amemmwagia sifa Wayne Rooney akisema kuwa nahodha huyo wa timu ya taifa ya England bado ana mchango mkubwa wa kutoa katika timu hiyo.

Nafasi ya Rooney katika kikosi cha England imekuwa shakani kutokana na mastraika Harry Kane na Jamie Vardy kuwa katika kiwango cha hali ya juu kabla ya fainali za Euro 2016.

Hata hivyo, mchezaji mwenzake huyo wa zamani wakiwa Manchester United, Ronaldo amesema kwamba mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30, ni tegemeo kwenye kikosi hicho cha Roy Hodgson.

Ronaldo na Rooney wana historia katika ngazi ya timu, ambapo Mreno huyo alisababisha Mwingereza kutolewa nje ya uwanja wakati wa fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2006.

"Mechi yetu dhidi ya England itakuwa kivutio kwangu kwa sababu ya Wayne Rooney na vitu vingine vingi. Rooney ni kiongozi na hilo sio jambo la kushangaza," staa huyo wa Real Madri aliliambia gazeti la Daily Mirror.

"Mara zote imekuwa ikinishawishi hata kuwa nyota wa England na tishio, nafasi ya unahodha inamfaa baada ya kumalizika dhama za kina David Beckham na John Terry," aliongeza staa huyo.


Comments