CHUMA KIMESAINI! ERIC BAILLY AANGUKA MIAKA MINNE MANCHESTER UNITED ...ndiyo usajili wa kwanza wa Mourinho Old Trafford
Eric Bailly amethibitshwa kuwa usajili wa kwanza wa Jose Mourinho ndani ya Manchester United baada ya kusajiliwa rasmi muda mfupi mara tu alipofuzu vipimo vya afya Old Trafford.
Beki huyo mwenye umri wa miaka 22 ambaye amecheza mechi 40 tu za mashindano makubwa katika historia yake ya soka, amejiunga na United kwa mkataba wa miaka minne kwa dau linalotajwa kufika pauni milioni 30.
Akizungumza baada ya kusaini United, Bally alisema: "Ni njozi iliyogeuka kuwa kweli kujiunga na Manchester United."
Eric Bailly akipozi na jezi ya Manchester United
Eric Bailly amesaini mkataba wa miaka minne United
Eric Bailly akipozi na jezi mpya ya mazoezi ya United baada ya kujiunga na klabu hiyo akitokea Villarreal ya Hispania
Comments
Post a Comment