CHRISTIAN BENTEKE KUTIMKA LIVERPOOL ASIPOHAKIKISHIWA NAMBA



CHRISTIAN BENTEKE KUTIMKA LIVERPOOL ASIPOHAKIKISHIWA NAMBA

CHRISTIAN BENTEKE amesema anataka kubaki Liverpool lakini ataondoka iwapo hatakuwepo kwenye mipango ya kocha Jurgen Klopp.

Mshambuliaji huyo alisajiliwa kwa pauni milioni 32.5 kutoka Aston Villa kiangazi kilichoipita lakini akashindwa kuonyesha makali yake.

Alifunga magoli 10 tu katika michezo 42 aliyocheza na mara nyingi akawa akitokea benchi kufuatia ujio Klopp mwezi Oktoba.

Bosi huyo wa Kijerumani alipendelea zaidi kuwatumia Divock Origi, Daniel Sturridge au Roberto Firmino kwenye safu yake ya ushambuliaji.
"Bado nina mkataba hapa na ningependa kubaki iwapo kocha ataniweka kwenye mipango yake"
Christian Benteke
Benteke ambaye bado ana miaka minne kwenye mkataba wake Liverpool, ataamua hatima yake baada ya Euro 2016.
"Katika umri wangu huu wa miaka 25 , sio kijana wala mzee lakini ni muhimu kucheza", alisema Benteke nyota wa kimataifa wa Ubelgiji.
"Bado nina mkataba pale na ningependa kubaki iwapo kocha ataniweka kwenye mipango yake.
"Kama haitakuwa hivyo, itakuwa vigumu kwangu kubakia Liverpool. Nitafikiria zaidi baada ya Euro," alisema katika mkutano wa waandishi wa habari.


Comments