BORUSSIA MONCHENGADBACH YAMFUNGA MIGUU RAFFAEL



BORUSSIA MONCHENGADBACH YAMFUNGA MIGUU RAFFAEL
TIMU ya Borussia Monchengadbach imemtia kitanzi staa wake, Raffael ambapo itashuhudiwa akiendelea kuitumikia klabu hiyo hadi mwaka 2019.

Mkataba wa sasa wa straika huyo mwenye umri wa miaka 31 ulitarajiwa kumalizika mwakani lakini sasa amefikia makubaliano ya kuendelea kuitumikia klabu hiyo ya Bundesliga.

Raffael alijiunga na klabu hiyo ya Borussia Park mwaka 2013 akitokea katika timu ya Dynamo Kiev na hadi sasa ameshafunga mabao 44 katika mechi 116 alizoichezea katika mashindano yote.

Msimu uliopita staa huyo raia wa Brazil alifunga mabao 13 na kutoa pasi za mwisho 10 katika mechi 31za Ligi.


Walikuwa ni wachezaji Robert Lewandowski, Pierre-Emerick Aubameyang, Henrikh Mkhitaryan na Thomas Muller ambao walimzidi mabao kwenye michuano hiyo ya Bundesliga.


Comments